
Klabu ya Azam Fc inapata ushindi mnono wa goli 3-1 ugenini dhidi ya Dodoma Jiji, magoli ya Saadun ’11 Feisal Salum ’45+3 kwa mkwaju wa penati na lile la kujifunga Dickson Mhilu ’60 yalipeleka alama 3 muhimu mitaa ya Chamazi.
Azam wanakwea mpaka kileleni mwa msimamo wa Ligi wakifikisha alama 30 baada ya michezo 13, ambayo ni michezo miwili zaidi ya Simba aliye nafasi ya 2 mwenye alama 28 na Yanga anayeshika nafasi ya 3 akiwa na alama 27.
Kama utani ila ndio hivyo Wanalambalamba wapo kileleni wanapigwa na baridi.


