
Chelsea na 4-2-3-1 na wakati wanaunda mashambulizi wanabadilika na kuwa 3-2-2-3 (Fofana/ Badiashile , Colwill na Cucurella kama CBs watatu nyuma then Caicedo anaingia ndani sawa na Lavia huku Enzo anasogea juu mstari mmoja na Palmer wanakuwa kama namba 8 / 10 wawili nyuma ya Sancho , Neto na Jackson …. Ehee baada ya hapo nini kilifuata ?
1 : Wale walinzi watatu wa Chelsea (Colwill , Fofana na Cucurella) wakati timu ikiwa na mpira walirahisisha kazi kwa pasi zao sahihi kufika kwa viungo wao wa chini Caicedo na Lavia ambapo Villa hawakufanya pressing nzuri kuweka presha kwa viungo hao rahisi kwa Chelsea .
2 : Chelsea walikuwa wanawalazimisha Aston Villa kuzuia eneo kubwa la uwanja kwa position za Neto na Sancho (ambao mda wote bila mpira wanakuwa pembeni kabisa ya uwanja kwenye mstari … maana yake wale Fullaback wa Villa wanalazimika kuzuia pembeni zaidi na space zinafunguka baina yao na mabeki wao wa kati .
✍️ Hapo ndio Palmer na Enzo walipopata nafasi kwenye mpira na nyuma ya kiungo cha Villa , tukaanza kuona Jackson anapata huduma kwenye eneo lake na form aliyonayo ni ngumu kuwaacha Villa (Yuko kwenye form bora msimu huu Magoli 8 mpaka sasa ) + goli la Enzo viungo wa Villa ni kama walikuwa watazamaji .
✍️ Kipindi cha pili , Nafikiri ni Chelsea wenyewe tu…. Walipata nafasi nyingi za wazi (Jackson , Sancho , Neto etc etc ) wangeweza kufunga zaidi ya magoli matatu , Villa walikuwa wazi sana tena unakutana na timu yenye mafundi kama Chelsea lazima wakuadhibu .
NOTE :
NICO JACKSON mpaka sasa kwenye Epl amefunga Magoli 8 + 3 Assist what a season kwa Nico
Enzo Fernandes “Back to Back” anafunga kwenye game za Epl ✅ !.. hii comb ya Lavia na Caicedo
Ollie Watkins kwa zile chance 1 vs 1 na Sanchez …. Leo Rodgers kapotezwa sana .
Palmer ✅ Cucurella , Colwill na Fofana / Badiashile ✅


