
Mwenye nidhamu kubwa ya kuweka akiba ya pesa huishi na mambo mawili. Mtu mwenye nidhamu ya kuweka akiba ya pesa, mambo mawili humuongoza katika safari yake ya mafanikio
1. Matumizi ya lazima
2. Matumizi ya muhimu
Matumizi ya lazima
Ni aina ya matumizi ambayo mtu mwenye nidhamu ya pesa au mtu yeyote akikosa hupata madhara na kuhatalisha maisha yake. Mifano ya matumizi ya lazima ni Chakula, malazi, mavazi (basic needs). Mtu mwenye nidhamu ya pesa huzingatia sana matumizi haya kuliko mengine nje ya hapo.
Matumizi ya muhimu
Matumizi ya muhimu ni aina ya matumizi ambayo akikosa au binadamu yeyote akikosa hapati madhara. Mfano Habari (tv & radio) n.k
Mwenye nidhamu ya kujisimamia na kutimiza malengo yake kwa kuweka akiba. Matumizi ya muhimu kwake sio kipaumbele cha maisha yake.
Hivyo hafanyi matumizi ya muhimu mpaka aweke akiba. Na hujaribu kupunguza matumizi ya lazima ili kukizi malengo yake.



