
Ally Shaban Kamwe baada ya kuhudumu kwa misimu miwili kama Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC ,leo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa mafanikio .
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kamwe ameandika
*A Good dancer must know when to Leave a Stage.
a ..
Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;
Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani.
Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu.
Muda wangu umemalizika na Asanteni sana.
Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa.
DaimaMbeleNyumaMwiko.
Mwenyekiti wa Wasemaji
Ally Kamwe.



