
Bahati mbaya kwa Boka, kama wanavyosema Waswahili, “Kamba hukatikia pabovu.” Wakati mashabiki wakiishutumu kwamba amezembea kuzuia bao, inasikitisha kusikia. Lakini tuchambue: nani angezuia na angefanya vipi? Pacome alijitolea kuzuia shuti lililopita mita chache tu, lakini bado bao lilitokea. Hivyo, kosa lake ni gani kweli?
Kuna wale wanaoshindwa kumkosoa kwa uwazi kwa sababu ya ustaa wake, lakini ukweli ni kwamba Pacome amekuwa na kipindi kigumu kiwanjani tangu mwanzo wa msimu huu. Kiwango chake kimekuwa cha wastani, tofauti na utegemezi mkubwa ambao mashabiki wanamuweka kwake.
Haikushangaza pale alipoanza nje Borge Al Arab dhidi ya Al Ahly, lakini taarifa zilisema kocha alikosea kumuanzisha nje kwa sababu Pacome ndiye mtu anayeogopwa na wapinzani. Lakini pale Zenji akaanza, hakuonyesha chochote cha kipekee. Wakati mechi Rabat jana, hakuonyesha “Fear Factor” zaidi ya mabeki na viungo wa kuzuia kufanya kazi ya kawaida hadi pale timu iliposhindwa.
Ukweli ni kwamba Pacome, kama wachezaji wengine wa nje, ni kipenzi cha mashabiki, hivyo hawezi kuchukuliwa lawama, lakini anapaswa kuwa makini na mchango wake kwa timu. Ukiwa na umri mkubwa kama mwanasoka, unapaswa kupunguza starehe, kuongeza mazoezi na kujitunza. Lakini Pacome anakula raha zaidi, akijua hatatachukuliwa lawama kama wenzake kama Boka, Duke Abuya, Dube, n.k.
Pacome ni “Fear Factor” na “X-Factor” katika Ligi yetu, hasa akicheza dhidi ya, Namungo, Mashujaa, Simba na timu nyingine, ambapo mashabiki wanampenda. Lakini kwa timu zilizoko kwenye hatua “waliyoaluka,” anapaswa kupunguza starehe, kufanya mazoezi zaidi na kujitunza ili kuhakikisha haiachi timu nyuma.
Mchambuzi Jemedari Said ameandika uchambuzi huu kupitia ukurasa wake wa Instagram, akisisitiza kuwa ingawa Pacome ni kipenzi cha mashabiki, ni muhimu kwa wachezaji wenye umri mkubwa kuzingatia mazoezi na nidhamu ya kibinafsi.

