
Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC imesema imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano na kutoa maneno ya kashfa pamoja na kauli zisizo na staha dhidi ya Mwekezaji wa Klabu hiyo, Ndugu Mohammed G. Dewji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bodi imesisitiza kuwa vitendo hivyo visivyo vya kiungwana havikubaliki na vinakiuka misingi ya heshima na maadili ya Klabu. Uongozi wa Simba SC umetumia fursa hiyo kutoa pole kwa Ndugu Mohammed Dewji kufuatia tukio hilo.
Aidha, uongozi wa Klabu umeeleza kuwa tayari umeliandikia Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika katika kuitisha mkutano huo, waliotoa kauli hizo au waliokula njama, kwa lengo la kuwafikisha katika vyombo vya dola kwa makosa ya jinai.
Bodi ya Wakurugenzi imeweka wazi kuwa haitabariki wala kuvumilia mtu yeyote atakayeharibu taswira ya Klabu ya Simba SC kwa namna yoyote ile.
Imetolewa na:
Crescentius Magori
Mwenyekiti
Bodi ya Wakurugenzi
Klabu ya Simba SC
05 Februari, 2026

