
Beki wa Klabu ya Simba SC, Charmou Karabou, amejiunga rasmi na Klabu ya TRA United ya Tabora kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita.
Hatua hiyo inalenga kumpa mchezaji nafasi ya kupata muda zaidi wa kucheza na kuendeleza kiwango chake cha ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Karabou anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha TRA United katika msimu unaoendelea, huku klabu hiyo ikiendelea kuimarisha safu yake ya ulinzi kuelekea michezo ijayo.

