
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta hapa nchini zilizoanza kutumika kuanzia leo Aprili 1, 2026, ambapo Petroli kwa Dar es Salaam imepanda kutoka Tsh. 2,864 hadi Tsh. 3,820 kwa Lita moja.
Maeneo kadhaa katika mikoa tofauti bei imepanda na kuwa zaidi ya Tsh. 4,000 kwa Lita moja ya Petroli baadhi ni Loliondo – Arusha, Geita (Tsh. 4,020), Kagera (Tsh. 4,080), Mara (Tsh. 4,038), Mwanza (Tsh. 4064), Busega – Simiyu (Tsh. 4,011).
Aidha, EWURA imesema mabadiliko hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran iliyoanza Februari 28, 2026 ikiwemo Iran kufunga Lango la Hormuz linalopitisha takriban Asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenye soko la Duniani.





