Neno moja lisilo sahihi kutoka kwako linaweza kuharibu uhusiano ulioujenga kwa miaka.
Huenda wewe si rafiki bora wa rafiki yako wa karibu{Best friend}.
Mtu yeyote atampa umuhimu zaidi yule anayempenda{whom he loves} kuliko yule anayempenda{who loves him}.
You would be replaced no matter what you are.
Hakuna furaha ya milele. Maisha yako yote utaendelea kujaribu kupata furaha moja baada ya nyingine. Kwa maneno mengine, kamwe hakutakuwa na kuridhika kabisa.
Kadri unavyokuwa na akili, ndivyo utakuwa na watu wachache wa kuzungumza nao kwenye kiwango chako.
Si uhimizo wote unaoupata ni wa kweli. Wakati mwingine mtu anakuambia hivi: ‘Ni wewe tu unayeweza kufanya hili’ ‘wewe ndiye mwenye ujasiri kati yetu..’ ‘ ili tu kukuweka mbele katika vita ili aweze kujificha nyuma yako. Ukishinda, atashiriki matunda. Ukishindwa, bado anaweza kusema: ‘Labda haikupaswa kutumia njia uliyotumia!!!’.
Baya lako moja ulilofanya kwa rafiki yako litafuta mambo 99 bora uliyowahifanya awali. Binadamu kwa kawaida wanachukulia uaminifu na wema kama kitu cha kawaida. Katika uhusiano, nia njema ya mtu inaonekana kama ubora wa msingi, sio faida.
Haijalishi unathibitisha vipi, watu walio karibu nawe wataamini wanachotaka kuamini.
Urahisi ni anasa. Kumfanya mtu aamini kwamba hauthamini pesa au pesa si kila kitu, unahitaji kupata pesa nyingi kwanza.



