” Mabinti wengi mna hiki kilio ; kinawatafuna ndani kwa ndani ”
Wengi mnaingia hapa kwasababu
1. Mna haraka sana ya kuolewa na mna shauku zilizopitiliza.
2. Wengi mnafikiri ukimvulia nguo kijana utayathibitisha mahusiano yenu.
3. Hutaki kumfanya huyo kijana ajisikie vibaya. Unahisi ukimpoteza umepoteza kila kitu.
4. Wengi mnaenda na hisia nyingi mnoo, hambakishi upande wa Roho Mtakatifu kuwaongoza.
5. Unahisi mahusiano hayo yakivunjika hautaolewa kabisa.
Mabinti muwe makini, watu wengi leo, sio watu halisi ; wengi huwadanganya kwamba nimeokoka, kumbe ni wajanja tu wa mtaani.
SASA UMESHAINGIA KWENYE SHIDA HII
( UMEACHIWA MAUMIVU )
Mambo ya kufanya
1. Jisamehe ( hauna cha kubadilisha hapo, zaidi ya kujibadilisha mwenyewe ndani) ; ameshauona uchi wako, hakuna kitu utabadilisha zaidi ya kujisamehe na kujiruhusu uendelee na maisha.
2. Angalia namna ulianguka, halafu jijenge kwenye eneo hilo. Kama wewe ni mtu wa hisia nyingi na unapenda mtu akujali sana, yamkini ulikuwa ndio mlango wa jambo hilo. Rekebisha hilo eneo, ili usije ukaongeza tatizo jingine.
3. Uwe na tumaini kwa Mungu kwamba; atakusaidia, na atakupa mtu sahihi, haijalishi uzoefu.
4. Usijirahisishe ; baada ya kuona umeanguka kwenye mtego huo. Wengi hujiona hawana thamani tena, kwahiyo anaanza kujiachia kwa kila mtu. USIFANYE HIVYO TAFADHALI.
5. Usilipize kisasi ; utaumia mwenyewe. Kwamba nataka ajue kwamba kuna watu wa maana wananipenda pia. UTAJIUMIZA ZAIDI.
6. Tafuta watu sahihi, ambao wataomba na wewe na kukufundisha hadi umeshinda na umevuka.



