️ : “Alivyokuwa United, huwezi kufikiria kuwa Cristiano Ronaldo angekuwa moja ya wafungaji bora zaidi katika historia,mechi yake ya kwanza dhidi ya Bolton. Alivyokuwa akijirusha, ilikuwa anakimbia na mpira na asijue wapi pa kuupeleka mpira,alikuwa kama mwenye kuchanganyikiwa, alikuwa akipiga chenga sana, kujirusharusha tu… mechi yake ya kwanza ilikuwa ngumu.
Kisha ghafla ikabadirika na ikabidi tu upitishe mpira kwa Cristiano. Hata katika timu yetu ambayo alikuwepo Tevez, Scholes au hata Rooney, yeye ndiye aliyeleta mabadiliko. Yeye ndiye aliyetuokoa tulipokuwa katika shida. Amekuwa mfungaji mabao, mtu anayeshinda mechi kwa kiwango cha juu zaidi.
Wachezaji wote wakubwa katika historia hufichuliwa wakati wa matukio makubwa. Alifanya hivyo kwa ajili yetu, kama alivyofanya kwa Real Madrid na Juventus. Ni uhakika: lazima achukuliwe kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote.”
CR7 ni bora kila wakati ❤️



