Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime inasema; “Disemba Mosi, 2024, majira ya saa nne na nusu usiku, Abdul Omary Nondo, ambaye alikuwa anatafutwa baada ya kukamatwa kwa nguvu katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, amepatikana akiwa ametupwa maeneo ya Coco Beach, Kinondoni, Dar es Salaam.”
Kwa mujibu wa taarifa, Nondo aliomba msaada wa bodaboda kufika Ofisi za Chama cha ACT Wazalendo, Magomeni, ambapo alikutana na viongozi wake na baadaye kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi wa afya yake.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini wahusika na chanzo cha tukio hilo, huku likiahidi kuchukua hatua za kisheria kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi.


