
Clement Mzize Nje ya Uwanja Hadi Mwisho wa Msimu Baada ya Upasuaji Afrika Kusini
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, Clement Mzize, atakuwa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji leo nchini Afrika Kusini.
Kulingana na taarifa zilizotolewa, Mzize amefanyiwa upasuaji huo kwa mafanikio na kwa sasa anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa madaktari. Hata hivyo, anatarajiwa kurejea tena uwanjani msimu ujao wa 2026/2027 baada ya kukamilisha programu ya matibabu na mazoezi ya kurejea katika ubora wake.
Jeraha hilo linamuweka nje ya kikosi cha Yanga SC katika kipindi muhimu cha msimu, hali inayowafanya mashabiki wa klabu hiyo kukosa huduma ya mshambuliaji wao tegemeo katika mechi zilizosalia.
Kwa ujumla, mashabiki, viongozi na wachezaji wenzake wamemtakia Clement Mzize uponaji wa haraka ili arudi akiwa na nguvu mpya zaidi.
Get well soon straika.




