

Klabu ya Yanga itashuka dimbani hii leo Februari 25, 2026 kukipiga dhidi ya timu ya JKT Tanzania katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es salaam.
JKT Tanzania atashuka katika mchezo huo akiwa ni kinara wa Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa akiwa na alama 26 katika michezo 16 aliyocheza msimu huu, huku Yanga akiwa na alama 23 na akiwa amecheza michezo 9 pekee.
Katika mchezo huu wa leo utakao wakutanisha Yanga dhidi ya JKT Tanzania, endapo yanga atashinda ataongoza msimamo wa Ligi kuu ya NBC akiwa na alama 28 huku akiwa amemzidi JKT Tanzania magoli ya kufunga na kufungwa.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye Ligi kuu ya NBC msimu uliopita Yanga waliibuka na ushindi wa Magoli 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.




