
Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Mchezaji Allan Okello mwenye umri wa miaka 25 raia wa Uganda kuwa Mchezaji mpya wa Yanga.
Okello anajiunga na Yanga SC akitokea Vipers SC ya Uganda, Msimu uliopita Okello alihusika kwenye magoli 23 ndani ya Klabu ya Vipers akifunga magoli 19 na kupiga pasi 4 za magoli (assist) na kufanikiwa kuwa mfumgaji bora kwenye ligi kuu ya Uganda 2024/2025
Allan Okello ni kijana mwenye nidhamu ya hali ya juu uwanjani na namba zinathibitisha hilo. Hajawahi kuonyeshwa kadi yoyote akiwa na jezi ya timu ya Taifa ya Uganda na katika ngazi ya klabu, hajawahi kupata kadi nyekundu huku akionyeshwa kadi za njano tatu tu tangu alipoanza kucheza soka la ushindani hadi sasa.
Okello ni zao la kituo cha kulelea vipaji vya soka cha klabu ya KCCA ya Uganda huku ikielezwa kuwa zimetumika Dola laki tatu kupata saini ya nyota huyo kutoka Vipers SC.



