Autodidacts ni neno la kiingereza linalomaanisha mtu kuwa na elimu bila kwenda shule/darasani. Wengine walienda kusomea vingine wakagundua wanapenda vitu ambavyo shule havipo wakaamua kuvibuni na kufikili leo ndio wamejaa kwenye makaratasi ya wasomi wetu wa leo.
Tujadili hawa wachache;
1:Sir Isaac Newton (mwanafizikia na mwanahesabu nguli)
Mtoto wa mkulima, tofauti na wengine Kidogo huyu alienda shule lkn alikuwa anasoma vitu vingine (philosophy)sio vile vilivyompa umaarufu. Upenzi wa hesabu aliupata alipojinunulia kitabu cha hesabu katika maonyesho. Newtons laws of motion, Formula nyingi za hesabu, uvumbuzi mwingi wa kisayansi tunaousoma kutoka kwa huyu jamaa alijifundisha na kubuni mwenyewe sio darasani. Leo watu wanakuwa maprofesor, wataalam kwa kusoma vitu hivi.
2.Malcom X
Huyu alijifundisha mwenyewe Philosophy, sociology na Genetics. Akiwa gerezani aliweza kuikopi dictionary yote kwa muda wa miaka saba na kuwa bora kwa misamiati iliyomfanya awe mwandishi na mzungunzaji bora. baadae alikuja kuwa mpiganiaji maarufu wa haki za binadamu na watu weusi.
3:Abraham Lincoln
Rais wa marekani mwenye heshima ya hali ya juu na Genius aliyeongoza taifa hilo bila uzoefu wa kutosha wa uongozi. Akiwa mtoto akizuiwa na baba yake mambo ya shule,kuna kipindi alikuwa anasafiri umbali mrefu kwenda kuazima kitabu ili ajisomee hukohuko shambani.bila huyu marekani leo ingekuwa vipande vipande, wazungu wengine walimchukia kwa kutetea watu weusi. Alitokea kijijini. Hakuwawh kwenda shule lakini alijifundisha mwenyewe sheria miaka mitatu. Huwezi kudefine neno Democracy bila kutoa kile alichokisema yeye.
4:ADOLF HITLER (mwanasiasa)
Hakumaliza shule ya sekondary kwa sababu ya uanaharakati. Alishindwa kujiunga chuo kusomea Ufundi sanifu kwa sababu hakuwa na vigezo (hakumaliza secondary). Baadae alitawal taifa la wasomi na kuisumbua dunia.
5:KARL MARX
(philosopher, economist, sociologist, journalist and
revolutionary socialist)
mjerumani mwenye asili ya uyahudi. Maisha yake mengi aliishi maktaba moja pale england akijisomea na kuandika concepts. watu walikuja kumuelewa baada ya kifo chake. leo sio tu watu tunajifunza aliyoandika, mchango wake uliigawa dunia katika itikadi mbili (ujamaa na ubepali)
6:Konstantin Tsiolkovsky
unapozungumzia Sayansi ya watu kenda mwezini. Huyu mrusi ndio mbabe na moja ya waanzilishi. Aliacha shule kwa kuwa alikuwa hasikii vizuri na wazazi kufariki. katika kujisomea akajikuta amependa physics na hesabu. Muda wake mwingi aliutumia maktaba kujisomea.Pamoja na kudharaulika duniani ukweli ni kwamba maandiko yake zaidi ya 400 yalileta mapinduzi makubwa katika sayansi ya kurusha rocket ulaya na marekani.
7:LEONARDO DA VINCI
(invention , painting, sculpting , architecture , science , music ,
mathematics, engineering, literature , anatomy, geology,
astronomy, botany , writing, history, and cartography )
Huyu ni kipaji maalumu, lkn vyote alijiendeleza mwenyewe. alikuwa na uwezo wa kuchora mkono wa kushoto wakati huohuo mkono mwingine anaandika.alikuwa anajua karibu kila kitu yaani super genius.
8:SOICHIRO HONDA
Huyu ndio HONDA mwenyewe. Ni msukumo na kiu ya kutaka kupata maarifa ndio iliyomsukuma kufanya mapinduzi ya kiviwanda maishani mwake na kuipa dunia zawadi ya Gari, Pikipiki na vifaa vingi vya magari.
9DAVID BEN GURION
Huyu ndio baba wa taifa na muanzilishi wa israel ya sasa. akiwa na umri wa miaka 18, aliachana na mambo ya shule akaanza kujisomea mwenyewe philosophy na kujifunza kigiliki kwa lugha asilia ili aweze kusoma vitu vingi katika uhalisia sio viivyotafsiriwa. Ndie aliyeanzisha mifumo yote ya israel ya sasa, ikiwepo vikosi hatari kabisa vya kijeshi. Alikuwa ahamini uwepo wa Mungu.
10:NIKOLA TESLA
Huwezi kuzungumzia mapinduzi ya sayansi bila kumtaja huyu mdau. Anamkono wake katika karibu kila kitu cha technologia. vitu ambavyo walisema haviwezekani leo vinawezekana. kwenye engine za ndege, telecom,IT, Magari, Rocket,Vifaa vya kijeshi, Umeme wa Maji etc. aliamua kuacha shule na kutengeneza workshop yake na kuanza kuvumbua vitu lukuki. Vitu alivyokuwa anafanya alisababisha watu wamuite MWANSAYANSI KICHAA. Ni baba wa AC ELectricity. Alikufa akiwa na ndoto ya kutaka kuusafirisha umeme kwenye anga ili dunia nzima umeme uwe bure. Katika majaribio yeke aliwahi kusababisha tetemeko la ardhi mji mzima. Leo japan na marekani wanafanya research kama wanaweza kutransmit electrical signals from US to Japan kwa kutumia Anga
11: Mwanamama KATO LOMB
Ni miongoni mwa watafsiri wa kwanza na pekee duniani mwenye uwezo wa kuafsiri lugha nyingi kwa mpigo (simultaneously Interpreter ). Alisoma degree ya CHemistry na Physics. Baadae akagundua upenzi wake sio hiyo vitu ni LUGHA. Akaamua kujifunza mwenyewe lugha zaidi ya 11 zilizomuingizia kipato kikubwa. Alijifunza kw akujisomea vitabu au novel za lugha husika hadi anaielewa kwa kuforce.
Formula yake ya mafanikio Aliyoibuni ni,
INVESTED TIME × MOTIVATION= RESULTS
INHIBITION
Aliweza kuongea na kutafsiri lugha zifuatao;
Bulgarian, Chinese, Danish, French, English, German, Italian, Hebrew, Polish, Latin, Romanian, Japanese, Spanish, Russian, Slovak, Ukrainian
12:BENJAMIN FRANKLIN
(one of the Founding father of USA, Inventor, scientist, politician, Musician, Deplomat, printer, entrepreneur,swimmer, writer, community worker na bbadae alijunga na kuwa freemason high degree, )
Aliandaliwa kuwa kasisi akiwa mtoto, aliacha shule akiwa na miaka 10 akawa anafanya kazi na baba yake kutengeneza sabuni na mishumaa, alippona haoni future aliamua kukimbilia kwa kaka yake mji mwingine ambapo alikuwa muuza magazeti na printer. akiwa 15 alienda england kufanya kibarua ndipo alipokutana na vuguvugu la mabadiliko ya fikra ulaya (the enlighment) hilo likamfanya awe na vyote hapo juu.
wengine;
Plato, Aristote,Galileo Galilei, Edger alan poe, Archimedes, Boyler, Bastian french economist (writter and idealists),Henry ford, Alexander Bell, Michael dell, Thomas Edison,
na wengine wengi.
makala kibao kuhusu watu hawa zimwshaelezewa kwenye page nikureview tu.



