
1. DUNIA INATAKA UBAKI MJINGA
Kadiri mtu anavyokuwa na uelewa mdogo, ndivyo inavyokuwa rahisi kwake kununua bidhaa na huduma bila kuzitathmini kwa kina.
Mfano: Watu wengi hutumia pesa nyingi kununua TV kubwa badala ya kuwekeza katika elimu au maarifa mapya.
2. USIIAMINI MFUMO WA ELIMU BILA KUFIKIRI
Mitaala ya shule na vyuo huwa imepitwa na wakati hata kabla ya mwanafunzi kuianza. Mfano: Unapofundishwa programu za zamani za kompyuta badala ya lugha mpya kama Python, unakuwa nyuma kimaendeleo.
3. SOMA BILA KUKOMA
Maarifa mapya yanaweza kuwa na manufaa wakati wowote.
Mfano: Kujifunza kuhusu uwekezaji mapema hukusaidia kuepuka matatizo ya kifedha baadaye.
4. JIFUNZE KUWASILIANA VIZURI NA WATU
Kujitenga na watu kwa kuwadharau kunaweza kukufanya ukose marafiki, wateja, au kazi.
Mfano: Mtu mwenye ujuzi mkubwa lakini hawezi kuwasiliana vizuri atakosa fursa nyingi kwenye maisha.
5.AIBU NI UPOTEVU WA MUDA
Kuruhusu hisia zikufanye ushindwe kufanya maamuzi ni kosa.
Mfano: Unaposhindwa kuuliza swali darasani kwa sababu ya aibu, unapoteza nafasi ya kuelewa Zaidi, au Kuwa na dhana wengine watakuchukuliaje au watasema nini kukuhusu…
6. USIPENDEZWE NA KITU KISICHOFAA KWENYE MAHUSIANO, KITAVUNJA MAHUSIANO YAKO
Tabia unayopuuza sasa itakuwa chanzo cha migogoro mikubwa baadaye.
Mfano: Ikiwa huwezi kuvumilia mtu asiye mwaminifu, usifikiri atabadilika baadaye.
7. ONGEA NA WAZEE MARA KWA MARA
Wazee wana hekima nyingi kutokana na uzoefu wa maisha.
Mfano: Kuongea na mfanyabiashara aliyefanikiwa kunaweza kukufundisha makosa unayopaswa kuepuka.
8. TAFUTA WATU WA KUWAIGA NA JARIBU KUWAPITA
Mfano: Ikiwa unavutiwa mtu aliyefanikiwa kwenye ujasiriamali, jifunze kutoka kwake na lengo lako liwe kumzidi.
9. KADRI UMRI UNAVYOSOGEA, WATU HUPENDA USALAMA ZAIDI
Hivyo, kama unataka kuchukua hatari kubwa, fanya hivyo ukiwa bado kijana.
Mfano: Uanzishe biashara ukiwa na miaka 25 badala ya kungoja miaka 50 ambapo utakuwa na majukumu zaidi.
10. USITUMIE PESA KWA UPUUZI
Badala ya kutumia pesa zako vibaya, ziweke akiba kwa mambo makubwa kama kuanzisha biashara.
Mfano: Badala ya kununua simu mpya kila mwaka, wekeza pesa hizo kwenye mradi wa kipato.



