

.
Kuna habari njema kwa Wananchi kutoka CAF ambazo zimewaumiza wenyeji wao US Monastir ya Tunisia.
.
Yanga imebakiza siku 9 kabla ya kupaa kuelekea nchini Tunisia kukutana na Monastir lakini wenyeji wao hao walikuwa wanapambana kuwapeleka wageni wao uwanja mmoja ambao ingekuwa ngumu kutoka salama kwa wawakilishi hao wa Tanzania katika shirikisho.
.
Monastir baada ya kuwapiga vibonde wa Yanga, Club Africain kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi, walijipanga kuhakikisha mchezo wao upigwe Uwanja wa Mustapha Ben Jannet.
.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia kurugenzi yake ya mashindano imewapiga stop! Monastir kucheza mechi dhidi ya Yanga katika uwanja huo wakiwaambia marekebisho waliyowaagiza kuyafanya hayajawaridhisha.



