Hapo Hrithik Roshan ana miaka 17, Babaake ndio Director wa Karan Arjun, na yeye ndio assistant..
Shah Rukh Khan na Salman Khan , wapo kwenye pick kubwa kuliko kawaida..
India ipo mabegani mwao, macho ya kila mtu, ni kuhusu wao na ustaa walionao..
Nani alimzingatia Hrithik Roshan kwenye picha hii, ambayo yeye ndio kaiomba?..
Miaka mitano mbele, historia inaenda kubadilika na kuandikwa upya..
Hrithik anacheza Kaho na Pyar hai, movie ya kwanza, tuzo 92 , we huogopi..
Nchi inatikisika, yule kijana aliekuwa hajulikani, sasa hivi yeye ndio hajui, kama kuna mtu hamjui..
Versatile actor , binadamu mwenye sura zaidi ya moja kwenye kioo..
Wanasema mpaka inachezwa Kabhi khushi kabhi gham, ilikuwa ni baada ya kuona Hrithik, amekuwa moto wa kuotea mbali.
Tasnia ikaamua kumchukua kakaake Shah Rukh Khan , kumuweka pembeni yake, zipigwe..
Kwa sasa Hrithik ni nani? mmoja wa waigizaji anaelipwa mkwanja mrefu India..
Kutoka kupewa hela ya Baba, kwa sasa akaunti inasoma dola milioni 370…
Kwenye steji ukitaka kushindana kucheza muziki, usihitaji Hrithik awe mpinzani wako, labda awe jaji..
Una haraka na maisha, unakata tamaa na hustle zako, angalia tena hii picha…
Hata wewe ni Hrithik wa jasho lako, lets push family..



